Ligi Ya WanawakeNyumbani
Simba Queens, Yanga Princess viwanja tofauti leo

MICHEZO mitano ya raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite inapigwa leo kwenye viwanja tofauti.
Simba Queens ni wageni wa The Tigers Queens kwenye uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu, mkoani Arusha.
Alliance Girls itakuwa wenyeji wa JKT Queens kwenye uwanja wa Nyamagana, Mwanza wakati Ceasiaa Queens ni wageni wa Baobab Queens kwenye wa Jamhuri, Dodoma.
Yanga Princess itaikaribisha Mkwawa Queens kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam huku Fountain Gate Princess ikiwa mgeni wa Amani Queens kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Nyangao, Lindi.