FANyumbani

Ni Azam vs Malimao ASFC leo

RAUNDI ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA inaendelea leo kwa michezo 7 kupigwa viwanja tofauti.

Azam ni wenyeji wa Malimao kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam wakati Rhino Rangers ni wageni wa Fountain Gate kwenye uwanja wa CCM Gairo, Morogoro.

African Lyon itaikaribisha Mbuni kwenye uwanja wa Chamazi huku Mbeya Road ikiwa mgeni wa Polisi Katavi kwenye uwanja wa Azimio.

Green Warriors itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye uwanja wa Isamuhyo wakati Stand itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Desemba 8 kumefanyika mchezo mmoja wa raundi hiyo ambapo COPCO ikiwa ugenini uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeichapa Silent Ocean mabao 3-2.

Related Articles

Back to top button