‘Avatar: Fire and Ash’ kuachiwa Desemba 19

LOS ANGELES: FILAMU mpya ya James Cameron, ‘Avatar: Fire and Ash’, imezinduliwa rasmi kwenye ukumbi wa Dolby Theatre, Hollywood, kwa ajili ya kuoneshwa kwenye kumbi za sinema ambapo watu maarufu na waandishi wa habari walihudhuria kwa wingi.
Uzinduzi huu pia ulihudhuriwa na wakosoaji wa filamu kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na baada ya kuangaliwa kwa filamu, maoni ya awali yamekuwa chanya kupindukia.
‘Avatar: Fire and Ash’, ambayo itaachiwa na kupatikana duniani kote rasmi Desemba 19, imepokelewa kwa shangwe huku wakipongeza muonekano wa picha za filamu, hadithi pana ya James Cameron, na jinsi filamu hii ilivyoandaliwa kwa ustadi mkubwa kama filamu za ‘Avatar’ za awali.
Jazz Tangcay wa Variety alimwambia James Cameron anainua kiwango cha ubora wa filamu. Hii ni kubwa zaidi, bora zaidi na yenye hisia zaidi kuliko zote. Ina picha za kuvutia, wahusika wapya wenye mvuto na ni kazi kubwa ya kiufundi.”
Courtney Howard, alikubaliana naye na kusema ‘Avatar: Fire and Ash’ ni “kama filamu ambazo zinajengwa kwa ajili ya sinema, “Filamu tatu sasa, James Cameron bado ana mbinu zake, anafanya filamu kubwa zionekane kwa hisia kubwa sana,” aliandika.
Mshambuliaji wa filamu, Sean Tajipour, alikiri kwamba hakuwa mpenzi mkubwa wa ‘Avatar’, lakini alikubali kwamba “James Cameron ana uwezo wa kuleta maonesho makubwa zaidi ya kiubunifu, akiongeza picha za kuvutia na hisia mpya.”
Peri Nemiroff wa Collider alishangaa jinsi filamu hii inavyoweza kuwarejesha watazamaji “Filamu tatu sasa, sijasita kusema kuwa filamu za ‘Avatar’ ni za kipekee na za kichawi sana.”
Filamu hii inaonesha wahusika kama Sam Worthington, Zoe Saldaña, Stephen Lang, Sigourney Weaver, Joel David Moore, CCH Pounder, Giovanni Ribisi, Dileep Rao, Matt Gerald, Kate Winslet, Cliff Curtis, na Trinity wakirudi kwenye majukumu yao kutoka kwa filamu za awali




