Muziki

Shoo za Burna Boy Marekani zawachanganya mashabiki

HOUSTON: MWANAMUZIKI nyota wa Afrobeats na mshindi wa Grammy, Burna Boy, amejikuta katikati ya mjadala mikali mtandaoni baada ya video kadhaa kutoka maonesho yake ya hivi karibuni nchini Marekani kuibua sintofahamu kuhusu mahudhurio.

Mwisho wa wiki, vipande vya video vilivyosambaa kwa kasi vilionesha sehemu za juu za ukumbi wa tamasha lake la Houston zikiwa na viti vingi vitupu, hali iliyosababisha mashabiki na wakosoaji kuhoji iwapo umaarufu wake umeanza kushuka.

“Burna Boy anapigwa vita sana na watu wanamcancel baada ya kuwafukuza mashabiki waliolala kwenye show yake huko Denver. Je, huu ndio mwisho wa safari yake ya muziki?” alihoijin mmoja wa mashabiki wake mtandaoni.

Hata hivyo, video nyingine zilizojitokeza mtandaoni zilionesha taswira tofauti kabisa. Katika baadhi ya vipande, ukumbi unaonekana uking’aa kwa mapambo huku sehemu za chini zikiwa zimefurika, mashabiki wakiimba na kucheza kwa shangwe na mshindi huyo wa Grammy.

Tofauti hizo za video zimewagawa mashabiki: wengine wakisisitiza kuwa tamasha lilikuwa na mahudhurio duni, huku wengine wakipinga vikali wakisema madai hayo yamezidishwa na hayalingani na historia ya Burna Boy katika soko la Amerika Kaskazini.

Mjadala huu unaibuka wakati msanii huyo bado akijadiliwa kutokana na kuwatimua katika shoo yake mashabiki waliokuwa wamelala huku wengine wakiburudika na shoo yake katika tamasha la Red Rocks Amphitheatre huko Denver.

Katika tukio hilo, Burna Boy alisitisha onesho katikati baada ya kumuona mwanamke aliyekuwa mbele kana kwamba amelala. Akizungumza na mwanaume aliyekuwa naye, alitoa amri kali:
“Mpeleke nyumbani… sifanyi wimbo mwingine mpaka mumuondoe.”

Baadaye iliripotiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa katika kipindi cha maombolezo ya msiba, jambo lililoibua hasira na ukosoaji mkali dhidi ya msanii huyo.

Akiwa chini ya moto wa maneno, Burna Boy alijibu kupitia livestream, lakini badala ya kutuliza mambo, alionekana kuongeza mafuta kwenye moto.
Alisema:
“Niliwaambia muwe mashabiki wangu? Nataka mashabiki wenye pesa kipindi hiki.”
Kauli hii ilizua mshtuko, kicheko na lawama kwa wakati mmoja, baadhi wakimtuhumu kwa kuwakataa mashabiki wake.
Hata hivyo, timu ya Burna Boy imepuuza madai ya mahudhurio duni, ikisisitiza kuwa ziara hiyo inafanya vizuri mno, ikiwa na maonesho mengi yameshauzwa na ratiba imeja hadoi mapema 2026.

Hadi sasa, takwimu rasmi za mahudhurio ya tamasha la Houston bado hazijaelezwa.

Burna Boy kwa sasa yuko katika ziara yake nchini Marekani ‘No Sign Of Weakness’, ambapo leo usiku atatumbuiza Dallas, Novemba 28 Minneapolis, kisha miji mingine kama Chicago kuelekea mwisho wa mwaka na atakamilisha ziara hiyo mapema mwaka ujao.

Related Articles

Back to top button