Mwakinyo: Mchanja yupo kamili kwa Mfilipino

MANILA: KOCHA wa bondia Yohana Mchanja, Khamis Mwakinyo amesema bondia wake yupo tayari kumvaa Mfilipino Regie Suganob Bingwa wa dunia wa WBO Global Jr. Flyweight katika pambano lisilokuwa la ubingwa litakalopigwa Jumamosi nchini Ufilipino.
Akizungumza na SpotiLeo Mwakinyo amesema tayari wameshawasili salama Ufilipino wakiwa katika hali nzuri na tayari kumvaa mpinzani.
“Tunashukuru Mungu tumefika salama Ufilipino, Mchanja yuko imara na timu yote ipo tayari na imejiandaa kikamilifu kwa ushindi kwenye pambano dhidi ya Mfilipino,”alisema.
Kwa upande wake Mchanja ameomba dua za watanzania ili kushinda pambano hilo la kimataifa. Mabondia hao wanatarajia kupima uzito kesho.
Mchanja mwenye nyota tatu amecheza mapambano 29 na kati ya hayo ameshinda 22, amepoteza sita na kupata sare moja. Takwimu za boxrec zinaonesha Mchanja hajawahi kushinda pambano nje ya nchi, huenda awamu hii amerudi kivingine.
Mpinzani wake amecheza mapambano 17 na kati ya hayo amepoteza moja. Hili litakuwa pambano lake la pili dhidi ya bondia wa kimataifa baada ya kuwahi kucheza na bondia kutoka Afrika Kusini na kupoteza




