CAF yamtuza Rais Samia kwa mchango katika michezo

RABAT: SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limemkabidhi tuzo Rais Dk Samia Suluhu Hassan, kutambua mchango wake mkubwa katika kukuza michezo hususan mpira wa miguu nchini.
Tuzo hiyo ilipokelewa kwa niaba ya Rais Samia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, katika hafla iliyofanyika Rabat, Morocco jana.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Wallace Karia, pamoja na Mwenyekiti wa Klabu za Afrika na Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said.
Kwa mujibu wa CAF, tuzo hiyo imetolewa kwa Rais Samia kama ishara ya kutambua jitihada zake kubwa katika kipindi cha utawala wake, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya michezo kama viwanja vikubwa, maandalizi ya mashindano ya CHAN, na maandalizi ya kuandaa mashindano ya AFCON 2027




