Kwingineko

UEFA yatoa kibali Camp Nou

BARCELONA: MABINGWA watetezi wa LaLiga, FC Barcelona, wamepokea idhini kutoka Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) kuruhusiwa kutumia uwanja wake wa Camp Nou, ambao unakarabatiwa, kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya (Champions League).

Hatua hii inajiri baada ya miamba hiyo wa Hispania kukaa zaidi ya miaka miwili ugenini kutokana na changamoto za ujenzi na kucheleweshwa kwa vibali vya usalama. Barcelona ilithibitisha kwamba UEFA imekubali ombi lao kwa kuwa masharti yote muhimu yametimizwa.

Mabingwa hao wa Hispania wataufungua uwanja huo kwa mara ya pili kwa mechi ya ligi kuu nchini humo dhidi ya Athletic Bilbao Novemba 22. Kisha, mechi ya kwanza ya Klabu Bingwa Ulaya itakuwa ni dhidi ya Eintracht Frankfurt Disemba 9, ikiashiria kurudi rasmi nyumbani.

Awali, Barcelona ilikabiliwa na changamoto, ikiwemo kulazimika kutumia Uwanja wa Mazoezi wa Johan Cruyff wenye uwezo mdogo mwanzoni mwa msimu, kabla ya kuhamia Uwanja wa Olimpiki wenye viti 55,000.

Kwa sasa, Camp Nou itafunguliwa kwa watazamaji 45,401 kwa muda. Ujenzi unatarajiwa kuendelea hadi kufikia uwezo kamili wa viti 105,000. Ucheleweshaji huu wa ujenzi unaathiri klabu kifedha, kwani inahitaji mapato ya uwanja huo, huku gharama za ujenzi upya zikikadiriwa kufikia Euro bilioni 1.5.

Related Articles

Back to top button