Mastaa

Salim na Salma Khan washerehekea miaka 61 ya ndoa yao

MUMBAI: SALIM Khan na mke wake Salma Khan wamefurahia siku yao ya kipekee kwa kusherehekea miaka 61 ya ndoa yao kwa hafla ya faragha iliyoandaliwa nyumbani kwao wakiwa na familia.

Sherehe hiyo ilijumuisha marafiki wa karibu na jamaa wa familia, ikiwa ni tukio la kipekee la kuonesha upendo na umoja wa familia hiyo maarufu.

Hali ilikuwa ya furaha tele nyumbani kwa Khan, wakati Salim Khan na Salma Khan wakiadhimisha miaka 61 ya ndoa yao, huku Arpita Khan na mumewe, Aayush Sharma, wakitimiza miaka 11 ya ndoa yao.

Familia haikukosa fursa ya kugeuza sherehe hiyo kuwa sherehe yenye burudani, ikiwashirikisha pia Salman Khan, msanii maarufu wa India.

Pia, malkia wa sinema Helen, mpenzi wa pili wa Salim Khan, alijiunga na sherehe hizo, akionyesha upendo wake kwa familia hiyo kubwa. Hafla hiyo ilijumuisha muziki, kucheza, kicheko na keki iliyochukua umaarufu mkubwa

Related Articles

Back to top button