Ligi Daraja La Kwanza

Aziz Andambwile ‘awashusha presha’ mashabiki Yanga

DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Klabu ya Yanga, Aziz Andambwile, amevunja ukimya na kuweka wazi ukweli kuhusu taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai kuwepo kwa sintofahamu kati yake na uongozi wa klabu hiyo.

Kupitia ujumbe wake kwa umma, Andambwile amesema bado ni mchezaji halali wa Yanga na kwamba haki zake zote za kimkataba tayari zimelipwa ipasavyo.

“Nipende kuchukua nafasi hii kuliweka sawa jambo linaloendelea mtandaoni kuhusu mimi na Klabu yangu ya Yanga. Mimi ni mchezaji wa Yanga na haki zangu za kimkataba tayari nilishalipwa,” amesema Andambwile.

Mchezaji huyo ameomba wanahabari kutumia vyanzo sahihi vya taarifa ili kuepusha taharuki kwa wachezaji na mashabiki wa timu mbalimbali nchini.

“Niwaombe ndugu waandishi wa Habari kuwa na vyanzo sahihi vya taarifa ili kutoleta taharuki kwa wachezaji kwenye timu zao,” ameongeza.

Andambwile alitumia nafasi hiyo kuwaomba radhi wote waliokwazika kutokana na sintofahamu hiyo, akisema:

“Niwaombe radhi wote ambao wamekwazika na sintofahamu iliyojitokeza. Asanteni.”

Related Articles

Back to top button