Kwingineko

Arda Güler azidi kujihakikishia nafasi

MADRID:KIUNGO wa Real Madrid, Arda Güler, anaendelea kuonesha kuwa msimu huu ni wake kweli. Msimu uliopita, alianza mchezo mmoja tu wa Ligi ya Mabingwa na hakupata dakika yoyote kwenye michezo ya mtoano. Lakini sasa, maisha mapya yamemfanya awe mchezaji muhimu mno kikosini.

Hadi sasa, amefunga mabao 4 na kutoa asisti 8 katika mashindano yote, na jana alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mchezo katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Juventus

“Najihisi muhimu sana katika timu hii msimu huu, na hii ni shukrani kwa kocha Xabi, ambaye daima ameniamini. Ananiambia niweke tempo ya mchezo. Ikiwa anataka nifungue au kutoa pasi ya bao, ananichezesha kama namba 10, kisha ikiwa anataka nisimamie tempo, ananichezesha kama namba 8,” alisema Arda.

Ni wazi kuwa Arda sasa ni mmoja wa wachezaji muhimu wa Real Madrid, akionesha kuwa kocha Xabi amemfanya aoneshe kiwango chake kikubwa msimu huu.

Related Articles

Back to top button