Muziki
Dully Sykes: “Mfalme wa Bongo Fleva ni Alikiba”

DAR ES SALAAM:MSANII mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes maarufu kama Dully Sykes, amethibitisha wazi kuwa Ali Kiba ndiye Mfalme wa muziki huo, na si mtu mwingine.
Akizungumza baada ya kuulizwa kama yeye ndiye King wa Bongo Fleva, Dully Sykes alionekana kushangazwa na swali hilo huku akitabasamu.
“Hapana, mimi sio Mfalme wa Bongo Fleva. Mimi ni muasisi wa Bongo Fleva. Mfalme anajulikana, Watanzania wote wanajua kwamba King ni Ali Kiba,” amesema Dully Sykes.
Kwa miaka mingi, Dully Sykes amehesabika miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva, huku akitambulika kwa mchango wake mkubwa katika kukuza tasnia hiyo.