Kwingineko

India yaingia tena kwenye 18 za FIFA

MUMBAI: India inaweza kufungiwa kutojihusisha na soka la dunia kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu baada ya FIFA na shirikisho la soka barani Asia kuitaka iwe na katiba mpya ifikapo Oktoba 30.

Shirikisho la soka duniani FIFA na Shirikisho la Soka la Asia (AFC) walituma barua ya pamoja kwa rais wa Shirikisho la Soka la India (AIFF), Kalyan Chaubey akielezea wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea kushindwa kukamilisha na kupitisha katiba.

“Kushindwa kutimiza ratiba hii kutatuacha tukiwa hatuna njia mbadala zaidi ya kupeleka suala hilo kwenye chombo husika cha maamuzi cha FIFA kwa ajili ya kuzingatiwa na kutolewa uamuzi,” ilisema barua hiyo iliyoonekana na AFP.

“AIFF lazima izingatie mawasiliano haya kuwa ya lazima na yanayohitaji ufuasi wa haraka ili kulinda haki zake kama mwanachama wa FIFA na AFC,” iliongeza.

Katiba ya AIFF imekuwa katika Mahakama ya Juu ya India ikisubiri uamuzi tangu 2017.

Kusimamishwa kunaweza kumaanisha timu za kitaifa na klabu za India kuzuiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa.

Awali FIFA iliisimamisha India Agosti 2022 kwa ushawishi wa mtu wa tatu baada ya Mahakama ya Juu kuteua kamati ya wasimamizi kuendesha AIFF.

Marufuku hiyo iliondolewa siku chache baadaye, na kufungua njia kwa AIFF kumchagua Chaubey.

Klabu ya soka ya ligi ya daraja la juu nchini India kwa sasa iko katika hali mbaya.

Ligi Kuu ya India (ISL) inaweza kusuluhisha mzozo kati ya AIFF na mshirika wake wa kibiashara.

Mchezo wa ISL wa msimu huu umecheleweshwa huku maelfu ya wachezaji na wafanyikazi wako katika hatari ya kupoteza kazi zao.

Mkataba wa haki kati ya AIFF na kampuni inayoendesha ISL, Football Sports Development Limited, unamalizika Desemba 8 na bado haujafanywa upya.

AIFF imeshindwa kuja na mpango wa kufufua ISL, ambao kwa kawaida huchezwa kati ya Septemba na Aprili.

Chama cha wachezaji FIFPRO Asia/Oceania kiliibua suala hilo na FIFA wiki iliyopita.

Related Articles

Back to top button