Moukoko aitwa kikosi Ujerumani Kombe la Dunia
						KINDA Youssoufa Moukoko ameitwa katika kikoci cha Kocha Hansi Flick wa Timu ya Taifa ya Ujerumani kwa ajili ya Kombe la Dunia ikiwa ni siku 10 tu kabla ya kutimiza miaka 18 baada ya kuonesha kiwango bora kwa wiki chache katika klabu ya Borussia Dortmund.
Moukoko alifunga mabao 2 katika ushindi wa mabao 3-0 wa Dortmund dhidi ya Bochum kwenye Bundesliga Novemba 5 na amekuwa mshambuliaji anayeanza mara kwa mara akimweka benchi Anthony Modeste aliyesajiliwa msimu huu.
Kikosi kamili cha Ujerumani kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zinazoanza Qatar Novemba 20 ni kama ifuatavyo:
Magolikipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre ter Stegen (FC Barcelona) na Kevin Trapp (Eintracht Frankfurt)
Walinzi: Armel Bella-Kotchap (Southampton), Matthias Ginter (Freiburg), Christian Gunter (Freiburg), Thilo Kehrer (West Ham), Lukas Klostermann (RB Leipzig), David Raum (RB Leipzig), Antonio Rudiger (Real Madrid), Nico Schlotterbeck (Borussia Dortmund) na Niklas Sule (Borussia Dortmund)
Viungo ni Julian Brandt (Borussia Dortmund), Leon Goretzka (Bayern Munich), Mario Gotze (Eintracht Frankfurt), Ilkay Gundogan (Manchester City), Jonas Hofmann (Borussia Monchengladbach), Joshua Kimmich (Bayern Munich) na Jamal Musiala (Bayern Munich.
Washambuliaji wa kikosi hicho ni Karim Adeyemi (Borussia Dortmund), Niclas Fullkrug (Werder Bremen), Serge Gnabry (Bayern Munich), Kai Havertz (Chelsea), Youssoufa Moukoko (Borussia Dortmund), Thomas Muller (Bayern Munich) na Leroy Sane (Bayern Munich).
				
					



