Gyokeres agoma kufananishwa na Henry

HONGKONG: Mshambuliaji wa Arsenal, Viktor Gyokeres amesema anataka kujitengenezea jina lake katika historia ya klabu hiyo na kupunguzilia mbali hoja za ulinganisho na gwiji wa klabu hiyo Thierry Henry baada ya nyota huyo kurithi jezi namba 14 iliyovaliwa na gwiji huyo.
Gyokeres alipewa jezi namba 14 iliyokuwa wazi ya Arsenal, ambayo nahodha wa zamani Henry aliivaa alipoweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo ya kaskazini mwa Jiji la London.

“Bila shaka najua kuhusu historia, Kusema ukweli hakukuwa na namba nyingi za za jezi na sikuwa na nafasi ya kuchagua hiyo (namba 14) ilikuwa inapatikana. Kwa hivyo nilipojua hilo ilikuwa chaguo rahisi kuichukua.” – Gyokeres aliviambia vyombo vya habari vya England baadaye Jumatano.
“Sio nia yangu kabisa kulinganishwa na kile Henri alichofanikiwa katika taaluma yake. Hasa hapa Arsenal. Nataka tu kufanya mambo yangu na kuonesha uwezo wangu. Bila shaka alikuwa mchezaji wa maajabu, lakini niko tofauti naye kabisa.” – aliongeza
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi mwenye umri wa miaka 27 ambaye alifunga mabao 54 katika mashindano yote msimu uliopita akiwa Sporting Lisbon alikamilisha uhamisho wake wa euro milioni 63.5 kutoka Sporting hadi Arsenal Jumamosi Jumamosi iliyopita.
Arsenal wataanza kampeni yao mpya ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United Jumapili ya Agosti 17 mwaka huu kabla ya kuvaana na Leeds United katika muendelezo wa Ligi hiyo pendwa zaidi Duniani.




