Mcheza Tenisi apigwa risasi na baba yake

INDIA: KATIKA tukio la kushangaza mcheza tenisi wa ngazi ya taifa Radhika Yadav mwenye miaka 25 raia wa India amepigwa risasi na babake huko Gurugram, Haryana.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea katika makazi yao huko Sushant Lok-phase 2.
Ameripotiwa kupigwa risasi na babake mzazi katika Gurugram ya Haryana leo.
Kulingana na taarifa ya awali, tukio hilo la kushtua lilitokea leo saa sita mchana katika makazi ya familia hiyo huko Sushant Lok-Phase 2 Sekta ya 57 ya Gurugram.
Kulingana na uchunguzi wa awali wa polisi wamesema, baba wa mshtakiwa alimpiga bintiye risasi tatu mfululizo alikimbizwa katika hospitali ya kibinafsi akiwa katika hali mbaya ambapo aliaga dunia kutokana na majeraha wakati wa matibabu.
Kulingana na vyanzo vya polisi, baba huyo alidaiwa kumuua bintiye kwa sababu inasemekana kuwa bintiye alikuwa na uhusiano na mtu ambaye hakukubaliwa naye.
Wakati huo huo, polisi wamemkamata baba mtuhumiwa na bastola iliyotumika katika kitendo hicho ilipatikana kutoka nyumbani. Chanzo cha uhalifu huo kwa sasa kinachunguzwa.
Radhika Yadav lilikuwa jina maarufu kwenye saketi za tenisi za ngazi ya serikali na alikuwa ameshinda medali kadhaa. Alikuwa mchezaji wa tenisi na aliendesha Chuo cha tenisi ambapo alitoa mafunzo kwa wachezaji wengine.




