Ligi Kuu

Job: Hatukubahatisha, tulipambana kwa malengo

DAR ES SALAAM: BEKI wa kati wa Klabu ya Yanga, Dickson Job ametaja siri ya mafanikio ya kikosi chao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25, akisema haikuwa bahati bali matokeo ya mshikamano na dhamira ya kweli ya kila mchezaji.

Jobo amesema hayo baada ya ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Kariakoo Derby uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Job amesema hali ya kupeana moyo miongoni mwa wachezaji ilikuwa nguzo muhimu katika kuimarisha morali ya timu kwa msimu mzima.

“Tulikuwa kitu kimoja, kila mmoja alimpa mwenzake moyo. Tulikumbushana kila wakati kuwa tuna lengo moja kuhakikisha tunaitetea heshima ya Yanga,” amesema.

Job amesisitiza kuwa wachezaji wa Yanga walikuwa na msimamo wa kupambania nembo ya klabu hiyo kongwe nchini.

Amesema walielewa thamani ya jezi wanayovaa na historia ya timu yao, jambo lililowasukuma kutoa asilimia mia kila walipoingia uwanjani.

“Tulikuwa tunapambana kwa ajili ya mashabiki wetu na historia ya timu. Hatuwezi kuvaa jezi hii bila kuwajibika. Tulijitolea kwa moyo mmoja,” amesema.

Job ameongeza kuwa walijua kuwa ushindi dhidi ya Simba ndiyo ungehitimisha ndoto yao ya kutwaa ubingwa msimu huu, waliingia kwenye mchezo huo kwa maelekezo mahususi na dhamira ya kuhakikisha wanapata ushindi muhimu uliowakabidhi taji la nne mfululizo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button