Filamu

Ridhi Dogra: Sitosahau nilipokuta na mastaa wa India

MUMBAI: STAA wa kike kutoka Bollywood, Ridhi Dogra amefunguka namna alivyowahi kupokea mwaliko wa kuhuduria onesho la mcheza filamu maarufu nchini India, Shah Rukh Khan ‘Saawariya’.

Katika mazungumzo ya wazi na Curly Tales, Ridhi Dogra ameeleza kwamba wakati alipokuwa akifanyakazi katika Televisheni ya Zoom, mwandishi wa habari za filamu Omar Qureshi alimpatia mwaliko yeye bila kujua anakwenda kukutana na mastaa wakubwa nchini India.

“Nilidhani ningeenda kutazama filamu tu, lakini nilichokutana nacho huko kilinishangaza maana mastaa wote wa tasnia nzima ya filamu walikuwepo, sitoisahau siku ile,” alieleza.

Amewataja waliohudhuria katika hafla hiyo wakiwemo magwiji, Amitabh Bachchan na Jaya Bachchan.
Mastaa wengine waliokuwepo katia hafla hiyo ni Rani Mukerji, Priyanka Chopra na Kareena Kapoor, Shah Rukh Khan na mtangazaji wa kwanza Deepika Padukone na Rekha

“Nilielemewa nilijihisi kama sikustahili kuwa pale. Hapo zamani, hatukupiga picha za selfie na nyota hao kulikuwa na hali ya heshima na aibu,” ameeleza.

Hata hivyo Ridhi Dogra ameonekana hivi karibuni katika mfululizo wa ‘JioHotstar Kull’, ambao ulianza kuonekana kupitia tv nchini humo Mei 2, 2025.

Related Articles

Back to top button