Hatimaye Wanawake Wenye Komwe wapata Mtetezi
Bien Asema “Siwezi Kuwa na Mwanamke asiyekuwa na Komwe”

NAIROBI:HATIMAYE wanawake wenye komwe wamepata mtetezi wao! Msanii maarufu kutoka Nairobi, Kenya Bien Aime Baraza (Bien), kutoka kundi la Sauti Sol amefunguka kuhusu mapenzi yake kwa wanawake wenye komwe.
Kupitia majibu kwa shabiki mmoja kwenye mitandao ya kijamii, Bien amesema wazi kwamba hapendezwi na wanawake wasio na komwe.
“Nawapenda wanawake wetu wenye komwe, siwezi kamwe kuwa na mwanamke ambaye hana komwe. Umemuona mke wangu?” alisema Bien akimrejelea mke wake Chiki Kuruka.
Kauli hiyo imekuja baada ya shabiki mmoja kumtania kuhusu wimbo wa Katam alioshirikishwa na Diamond Platnumz, akidai Bien amekuwa akiimba kuhusu wanawake wa Kenya wenye komwe.
Bien hakusita kumwaga hisia zake na sasa wanawake wenye komwe wana kila sababu ya kutembea kifua mbele!