Ligi Daraja La Kwanza

Ligi ya wavu Zanzibar kuanza Okt 30

LIGI Kuu ya mpira wa wavu Zanzibar inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 30, 2022.

Ligi hiyo itakayoshirikisha timu 11 zikiwemo saba za wanaume na nne za wanawake,
itachezwa katika Kisiwa cha Pemba katika Uwanja wa Tenisi, Chake Chake.

Akizungumza na gazati la HabariLEO Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Chama cha
mchezo huo Zanzibar (Zava), Burhan Ali amesema kwamba wamejiandaa kuanza kwa ligi
hiyo ili iwe katika mafanikio mazuri.

Amesema katika ligi hiyo ambayo itashirikisha timu 11, tisa kutoka Unguja ambapo nne
kati yao ni za wanawake na tano za wanaume na timu mbili zote zikiwa za wanaume ni za
Pemba.

Burhan amezitaja timu hizo ni pamoja na Polisi, Mafunzo, Nyuki, KVZ na JKU na kwa
wanawake ni JKU, KVZ, KMKM na Mafunzo na za Pemba ni Mkoroshoni na Micheweni.

Alisema matarajio yao katika ligi ya msimu huu itakuwa nzuri kutokana na kila timu kujipanga kwa ushindani.

Related Articles

Back to top button