Mastaa

Kylie Jenner ampiga marufuku mpenzi wake kuigiza mapenzi katika filamu

CALIFORNIA: MSHIRIKI wa vipindi vya runinga vya ‘The Kardashians’ na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Kylie Jenner amempiga marufuku mpenzi wake ambaye ni muigizaji wa filamu Timothee Chalamet kuigiza nafasi za kimapenzi katika filamu atakazoshiriki.

Mrembo huyo ameonekana kutoridhika na Timothee kutokana na ukaribu na kucheza nafasi ya kimahusiano kwa ufasaha zaidia kiasi kwamba anadhani kuna kinachoendelea na wasichana anaocheza nao baada ya filamu hizo kukamilika.

Wadau wa filamu wanasema kuwa mrembo huyo ameona wivu anapomuangalia mpenzi wake huyo katika filamu ya ‘Call Me By Your Name (2017)’ alivyoshiriki katika matukio ya kimapenzi na washiriki wengine.

Hata hivyo Timothee amekuwa kimya huku wadau wa sanaa na mashabiki wake wakisubiri kuona kama atafanya uamuzi wa kufuata taaluma yake ya uigizaji ama kauli ya mpenzi wake.

Kylie Jenner aliyezaliwa Agosti 10,1997 huko Los Angeles, California, nchini Marekani na mpenzi wake Timoth wapo katika uhusiano wa kimapenzi kwa takribani miaka miwili sasa.

Related Articles

Back to top button