Ligi Ya Wanawake

Dk Stergomena awapa tano JKT Queens

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Stergomena Tax ameipongeza timu ya JKT Queens, kwa kutwaa kikombe cha ubingwa wa mashindano ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (WPL).

Dk Stergomena ameupongeza uongozi wa JKT, chini ya mkuu wake, Rajabu Mabele, kwa kuisimamia vema timu hiyo na kuwezesha mafanikio hayo makubwa, yanayoiheshimisha JKT.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa timu za JKT, Masau Bwire, Dk Stergomena amesema kadiri muda na nafasi utakavyoruhusu atapanga kuonana na timu nzima ya JKT Queens ili kuwapongeza Zaidi.

JKT Queens ilitwaa ubingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa baada ya kulingana pointi sawa na Simba Queens yaani 47.

Ilimaliza mzunguko wa mechi 18 ikiwa kinara ikishinda michezo 15, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja saw ana Simba. Ilitofautiana mabao ya kufunga ambapo ilifunga mabao 69 na kufungwa saba huku wapinzani wao wakifunga 57 na kufungwa 15.

Timu hiyo sasa imefikisha idadi ya mataji manne saw ana waliyokuwanayo Simba Queens. Mara ya mwisho JKT kubeba taji hilo ilikuwa mwaka 2023 na mengine ilichukua mwaka 2017/2018 na 2021/2022.

Related Articles

Back to top button