Nyumbani

Fainali ya Simba vs Berkane kuchezwa kwa Mkapa

DAR ES SALAAM:NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ‘Mwanafa’ amesema mchezo wa Simba dhidi ya Berkane ya Morocco utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kutua na kikosi Cha wekundu hao akitokea Afrika ya Kusini Mwinjuma amesema maelekezo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kwamba wao hawatakiwi kuwa kipangamizi, kwa namna yoyote wanayoweza kulifanya Simba ikawa na mazingira rafiki na wao wakaweza kushinda watafanya.

“Tunashukuru serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapokea Simba kwenye hatua ya nusu fainali, jambo hilo linaonesha mahusiano mazuri katika pande mbili za Muungano, Wazanzibar nao walitaka kuona hatua kubwa kama ile inafanyika kwenye ardhi yao,

“Lakini Uwanja wa Zanzibar una uwezo wa kuingiza watu 15,000 ukilinganisha na Benjamin Mkapa Unaoingiza watu 63,000 kwa hiyo tunataka kuwapa nafasi Watanzania wengi zaidi kushuhudia mchezo huu kwa macho yao wenyewe,”amesema.

Amesema wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha marekebisho ya Uwanja huo yanakamilika kwa muda ili Simba watumie Uwanja huo kwa fainali Mei 25, mwaka huu.

Mwinjuma amesema leo atakagua Uwanja huo kuangalia maendeleo ya marekebisho yake na kutoa maelekezo ya nini kifanyike.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button