Serie A

Penati kuamua bingwa Serie A msimu huu?

MILAN:UWEZEKANO wa bingwa wa ligi kuu ya Italy Serie A kuamuliwa kwa mchezo wa Playoff au hata mikwaju ya penati unazidi kuwa mkubwa baada ya farasi wawili wanaoongoza mbio za kuwania ubingwa huo kufungana kwa idadi ya pointi huku kukiwa kumesalia michezo mitano pekee kukamilisha msimu huu.

Mabingwa watetezi Inter Milan na SC Napoli wamefungana kwa idadi ya pointi 71 baada ya michezo 33 Inter wakiwa kileleni kwa tofauti ya idadi ya mabao ya kufungwa na kufunga lakini kigezo hiki hakutatumika ikiwa mambo yataisha kama ilivyo sasa.

Ubingwa wa Serie A umeamuliwa kwa playoff mara pekee ikiwa ni Juni 7 mwaka 1964 baada ya Inter Milan kufungana na Bologna kwa idadi ya pointi 54 na Inter wakapoteza ubingwa kwa Bologna baada ya kipigo cha 2-0 katika uwanja wa Stadio Olimpico uliopo katika mji mkuu wa nchi ya Italy, Rome.

Mwaka 2005 ligi hiyo iliuondoa rasmi mfumo wa playoff kisha kuamua bingwa apatikane kwa head-to-head na tofauti ya magoli yaani goal difference ikiwa timu moja au zaidi zitakuwa na idadi sawa ya pointi kwenye msimamo lakini hii haijawahi kutumika.

Serie A iliurudisha tena mfumo wa Playoff mwaka 2022 na Napoli akatwaa taji la ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 16 huku Inter wakitwaa msimu uliopita kwa gepu la pointi 19. Sasa timu hizi mbili ziko kwenye harakati za kutafuta ufalme wa Serie A msimu huu.

Inter Milan walikalia kilele cha ligi mwezi februari wakitanua uongozi wao kwa pointi tatu lakini yote yalibadilika wikiendi iliyopita baada ya Napoli kushinda 1-0 kwa Monza na Inter kupotea 1-0 dakika za jioni mbele ya Bologna. Ikiwa inter wataendelea kuwa na uwiano mzuri wa mabao watapata faida ya mchezo wa playoff kuchezwa nyumbani kwao. Mchezo huu utachezwa kwa dakika 90 pekee kisha mikwaju ya penati kama matokeo yatakuwa sare.

Related Articles

Back to top button