Kwingineko

“inabidi mnivumilie tu, hakuna namna” – Postecoglou

FRANKFURT, KOCHA mkuu wa Tottenham Hotspur Ange Postecoglou amesema mashabiki klabu hiyo hawana budi bali kumuamini na kumvumilia kwa kipindi kirefu kidogo na kuwaahidi kuwa project aliyoiandaa inaelekea kuzaa matunda hivi karibuni akianza na kutinga hatua ya Nusu fainali ya michuano ya Europa League usiku wa kuamkia leo.

Postecoglou ambaye jumatano alisema hana uhakika na kibarua chake ikiwa atashindwa kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kupata sare ya 1-1 katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Europa League dhidi ya Eintracht Frankfurt wiki iliyopita ameivusha Spurs kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya ushindi wa 1-0 ugenini.

“Mashabiki wetu wamepitia magumu mengi, natumai ushindi huu utawapa tumaini jipya. Mimi ni Kocha yule yule wa siku zote. Wachezaji hawajapoteza imani kabisa, wanaobeza mafanikio yetu tuachane nao”

“Binafsi sijali hainisumbui wala haina athari hata kidogo kwenye mipango yangu, kaazi yangu ni kuhakikisha kuna morali kwenye dressing room kama staff na wachezaji wananiamini inatosha hiyo ni muhimu kuliko maoni ya mtu mwingine yeyote hakuna namna itabidi mvumilie tu kwa muda mrefu kidogo” – amesema Postecoglou

Spurs hawana mwendo mzuri msimu huu na mashabiki wengi wat imu hiyo wamepoteza Imani ya kikosi hicho kufanya vizuri wakiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ya England, huku uongozi wa klabu hiyo ukipambana kukinusuru kikosi hicho kumaliza nafasi ya chini zaidi kwenye historia ya klabu hiyo tangu mwaka 1994

Ushindi mbele Eintracht Frankfurt na kufanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali unafufua tumaini jipya kwa mashabiki wa klabu hiyo ya London na sasa nguvu yao huenda ikatumika zaidi kwenye kutwaa kombe hilo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button