Kwingineko

Mbappe afurahia uzinduzi wa sanamu lake London

LONDON: SANAMU la nyota wa soka wa Ufaransa Kylian Mbappe limezinduliwa jijini London likiwa katika umbo la nyota huyo ikiwa ni moja ya heshima kubwa zaidi ambazo Uingereza imempa mwanaspoti kutoka taifa linguine.

Sanamu hiyo imezinduliwa katika makumbusho ya Madame Tussauds ya London nchini Uingereza.

Sanamu hiyo inamwonyesha mshindi wa Kombe la Dunia la 2018 akipiga pozi alilolizoea la kupitisha mikono kifuani kwake likiwa limevalishwa jezi nyeupe ya ugenini ya Ufaransa iliivaa katika Mashindano ya Uropa msimu uliopita pia anaonekana akiwa amefunga kitambaa cha unahodha.

“Nguo nzima … ilitolewa na Mbappe mwenyewe,” Madame Tussauds alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Sanamu hiyo ilionyeshwa hadharani katika ukumbi wa katikati mwa London jana Aprili 4, 2025, na kumuona Mbappe akichukua nafasi yake pamoja na wasanii wengine nguli wa kandanda wenye masanamu akiwemo Pele na Cristiano Ronaldo.

“Wacha nikutambulishe kwa pacha wangu,” alitania kwenye chapisho kwenye Instagram.

Jo Kinsey, meneja wa studio kwenye jumba la makumbusho, alisema amefurahishwa na majibu ya Mbappe.

“Ilikuwa ya kushangaza. Alisema aliheshimiwa lakini kwa kweli tumeheshimiwa,” aliiambia AFP.

Waandaaji wa sanamu hilo wamedai walichukua mamia ya vipimo na picha ili kukamata kwa usahihi rangi ya nywele, ngozi na macho yake, alisema Kinsey, akiongeza kuwa hata uchunguzi wa meno ulitumia muda mwingi kufanya utafiti kujua nini waweke.

“Tulijadili pozi, sura,” aliongeza.

Mbappe, 26, tayari ana sanamu zenye mfanano wake huko Madame Tussauds, Berlin na Musee Grevin huko Paris.

Related Articles

Back to top button