Filamu

Kidole cha mtoto champonza Hemsworth

JAPAN: MCHEZA filamu za mapigano, Chris Hemsworth amejikuta matatani baada ya mashabiki wake kukerwa na moja ya picha alizoposti katika ukurasa wake wa Instagram akiwa mapumzikoni na familia yake nchini Japan.

Staa huyo akiwa na mke wake, ambaye ni muigizaji na mwanamitindo kutoka nchini Hispania, Elsa Pataky wakiwa na watoto wao watatu binti India Rose na mapacha Sasha na Tristan wakiwa eneo lenye theluji nchini humo mmoja wa watoto hao anaonekana kunyanyua kidole kinachoashiria tusi na kuzua mjadala mtandaoni.

Mashabiki wa staa huyo wa ‘Extraction 1&2’, ‘Spiderhead’, ‘Furiosa A Mad Max Saga’ na nyingine nyingi wamewataka mastaa duniani kote wawafunze watoto wao mambo yanayofaa kuonesha katika picha na video wanazochukua wanapokuwa katika nchi za nje.

Lakini pia mashabiki hao wamemjia juu staa huyo kwa kupuuza tusi la mtoto wake akiliposti huku akijua si ishara nzuri na inaweza kumkosanisha na mashabiki wake kama ilivyotokea.

“Huyu msanii naye ni changamoto alijua kabisa ishara aliyoonesha mtoto wake ni ishara mbaya lakini bado aliposti picha hiyo inakera mno inakwaza na imetuchukiza mashabiki wake. Hawa mastaa wanatakiwa wawafunze Watoto wao mambo ishara za matusi na kibaguzi kwani zinaweza kuwaletea matatizo makubwa tofauti na wanavyodhani,” amesema mmoja wa mashabiki hao.

Hemsworth na Pataky walifunga ndoa kimya kimya wakati wa sikukuu za Krismasi mwaka 2010, waliwakaribisha watoto wao miaka mitano baadae.

Related Articles

Back to top button