Tetesi

Chelsea yavuna wawili kwa Amorim

LISBON, Klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno imethibitisha kuwauza winga wake Mreno Geovany Queda na kiungo Dario Essugo kwenda Chelsea kwa dau la kitita kinachoweza kufikia Euro milioni 74.4

Tayari Chelsea imekubali kulipa dau tangulizi linalofikia euro milioni 52 kwa Queda mwenye miaka 17 raia wa Ureno mzaliwa wa Guinea-Bissau ambaye pia alikuwa kivutio cha Manchester United baada ya kinda huyo kukulia chini ya mbawa za Ruben Amorim hapo Sporting.

Wakati huo Essugo mwenye miaka 20 alieanzia soka la kulipwa katika klabu hiyo ambaye kwa sasa anakipiga LaLiga kwenye klabu ya Las Palmas anatarajiwa Stamford bridge majira ya joto kwa dau la Euro milioni 22.2.

Wenyeji hao wa Stamford bridge wako katika harakati za kujiimarisha ili kurejesha makali yao msimu ujao baada ya kupoteza makali yao msimu huu wakigombania nafasi ya kuwa kwenye michuano ya kimataifa hususan ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button