Filamu

Zoe Saldaña atokwa machozi baada ya kushinda Oscar ya Kwanza

LOS ANGELES: MCHEZA filamu Zoe Saldana ametokwa na machozi alipopokea Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike katika Tuzo za Oscar zilizotolewa Usiku wa Machi 2, 2025 katika Ukumbi wa Dolby huko Los Angeles nchini Marekani.

Muigizaji huyo mwenye miaka 46 amesema: “Nimefurahi mno kushinda tuzo hii ya Oscar kupitia filamu ya ‘Emilia Perez’ nikishindanishwa na Monica Barbaro, Ariana Grande, Felicity Jones na Isabella Rossellini”.

Katika hotuba yake alimshukuru Mama yake: “Mama! Mama! Mama yangu yuko hapa, familia yangu yote iko hapa. Nimefurahishwa na heshima hii.

“Asante sana Academy kwa kutambua uwezo wa mwanamke kama Rita na kuzungumzia wanawake wenye nguvu, wateule wenzangu, upendo na jamii mliyonipa ni zawadi ya kweli na nitailipa. Asante sana. Kwa waigizaji wangu na kikundi cha ‘Emilia Perez’, ninashiriki tuzo hii nanyi,

Pia aliwashukuru washiriki wenzake na kampuni anazofanyia kazi: “Netflix, Ted, Lisa, Bella, YSL, asante kwa msaada wako. Kwa timu yangu huko CAA, mameneja na wanasheria wangu wote na wanawake wenye nguvu na asante kwa kila mtu.

Zoe ana mapacha wenye umri wa miaka 10, Cy Bowie na Zen,ameolewa na Marco Perego ameendelea kuwashukuru mama na baba yake Pamoja na familia yao kwa ujumla akidai kwamba lolote lililowachukiza kutoka kwake alifanya kwa ajili yao.

“Na kwa mume wangu, una nywele nzuri, wewe ni… Heshima kubwa maishani mwangu umekuwa mshirika wangu na wana wetu warembo, Cy Bowie na Zen, wanajaza anga zetu kila usiku na nyota,

“Bibi yangu alikuja nchini mwaka wa 1961, mimi ni mtoto wa kujivunia wa wazazi wahamiaji mwenye ndoto na heshima nimefanya bidii mno na mimi ni Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Dominika kupokea Tuzo ya Academy na najua sitakuwa wa mwisho. Natumai kuwa ninapata tuzo kwa jukumu nililopata kuimba na kuzungumza kwa Kihispania, bibi yangu kama angekuwa hapa, angefurahishwa sana. Asanteni sana.” Alimaliza Zoe aliyetamba katika filamu mbalimbali zikiwemo Avatar na Avengers.

Related Articles

Back to top button