Simeone roho juu kwa Valencia

MADRID, Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ameonesha wasiwasi wakee juu ya uwezo unaooneshwa na wapinzani wake wa wikiendi hii Valencia akieleza kuwa wapinzani hao ni wagumu kwakuwa wamekuwa wakiimarika kila siku.
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari Simeone amesema wanaowafuatilia vijana hao wameona kuwa sio timu ya kubeza hata kidogo.
“Kama mmewaona Valencia tutakubaliana kuwa wamekuwa wagumu na wanaimarika kila kukicha, na wakiwa nyumbani wanakuwa na faida zaidi kwa sababu wana mashabiki wao. kwa upande wetu tumekuwa na bahati sana kupata mechi nyingi muhimu, tutauleta moto wetu huku kwa kuanza na Valencia” amesema
Atletico Madrid walio katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Laliga pointi moja tu nyuma ya vinara Barcelona watakuwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya Valencia katika dimba la Estadio de Mestalla kusaka ushindi baada ya sare mbili mfululizo.
Valencia hawajapoteza katika michezo yao mitatu iliopita na watapambana kuendeleza wimbi hilo la ushindi. katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Metropolitano Atletico walishinda 3-0 mwezi Septemba mwaka jana.




