Ligi Kuu

We Fadlu utaua watu ujue!

DAR ES SALAAM: KAMA ulidhani Simba wamemaliza basi unajidanganya mtu wangu! Unaambiwa kazi ndio kwanza imeanza timu inaendelea kusukwa, hii ni baada ya kauli ya kocha wa Simba Fadlu Davids kuwa bado hajakamilisha kuitengeneza timu anayoitaka.

Kocha huyo ambaye aliingoza Simba kushinda mabao 5-2 dhidi ya Kagera Sugar juzi Jumamosi amesema licha ya matokeo mazuri wanayopata kwasasa bado hajaridhishwa na timu yake.

“Hii sio namna ambayo tunatakiwa kuwa, ni lazima tuoneshe ukubwa wetu, ninafurahishwa na jinsi wachezaji wanavyojituma kwaajili ya hii timu lakini bado hawajaonesha ukubwa ambao timu inapaswa kuonesha, tunaendelea kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali na muda ukifika wanasimba wataelewa nini namaanisha” amesema Fadlu

Ikumbukwe kwamba mpaka sasa Simba ndio vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa wamevuna pointi 34 katika michezo 13 waliyocheza wakishinda michezo 11 sare moja na kupoteza mchezo mmoja pekee.

Aidha Simba ndio timu iliyofunga mabao mengi zaidi kwenye ligi hadi kufikia sasa wakiwa wamefunga mabao 29 mengi kuliko timu nyingine zote na kuruhusu mabao matano pekee machcahe zaidi kuliko timu nyingine kwenye ligi.

Pia kabla ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar Simba ilicheza michezo sita bila kuruhusu nyavu zake kuguswa lakini licha ya kuwa bora katika maeneo yote hayo kocha Fadlu anasisitiza kuwa bado hajakamilisha kuijenga timu yake.
Desemba 24 Simba watashuka tena dimbani kuwaalika JKT Tanzania katika Uwanja wa KMC, uliopo Mwenge Dar es Salaam.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button