KLABU ya Dodoma Jiji leo imeondoa ukame wa ushindi katika michezo ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara msimu 2022/23 baada ya kuifunga Geita Gold kwa bao 1-0.
Bao hilo pekee la Dodoma Jiji limefungwa na Collins Opare katika dakika 30 kwenye uwanja wa Liti mjini Singida.
Dodoma Jiji sasa imefikisha pointi 5 baada ya michezo 5 wakati Geita Gold imebaki na pointi 3 baada ya idadi kama hiyo ya michezo.




