Fadlu, Gamondi wanaitaka mechi

DAR ES SALAAM: HOMA ya mchezo wa Kariakoo Dabi Simba vs Yanga imeanza kupanda, zikiwa zimesalia siku 2 tu kupigwa kwa mchezo huo unaovuta hisia kali za mashabiki wa soka nchini na Afrika kwa ujumla.
Joto kali limehamia kwa makocha wa timu hizo mbili, Fadlu Davids kwa upande wa Simba na Miguel Gamondi kwa Yanga.
Fadlu Davids, amesisitiza nidhamu ya kiufundi na kiakili, wanajua ubora wa Yanga, lakini wamejiandaa kimkakati wawe makini kwa kila dakika ,kujenga mashambulizi kwa kasi na safu ya ulinzi kuwa na umakini mkubwa.
“Katika mechi hizi nafasi ni chache, tunahitaji kuwa bora katika nafasi zinazopatikana katika kumalizia kutafuta ushindi,” amesema Fadlu.
Kwa upande wa kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ambaye amekuwa mwiba mchungu kwa Simba baada ya kuwapiga mara tatu, kwenye michezo miwili ya ligi kuu msimu uliopita na Ngao ya Jamii msimu huu amesema kuwa kikosi chake kipo vizuri kuelekea mchezo huo.
“Simba ni timu kubwa yenye wachezaji wenye vipaji vikubwa na historia ya mafanikio, tunawaheshimu sana kama wapinzani, tunajipanga vizuri kwa mchezo huu,” amesema kocha huyo.