Nyumbani

Kumbe Azam FC ni kitoto cha 2000

DAR ES SALAAM: MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa presha wanayokutana nayo kati ya Azam FC ni tofauti na dabi ya Kariakoo.

Ahmed ameyasema hayo kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao wakubwa , Yanga SC ,Oktoba 19 katika dimba la Benjamin Mkapa, saa 11 jioni.

“Mechi ya Jumamosi (dhidi ya Yanga ) ni tofauti tunapokutana na timu kama Fountain Gate FC,  Singida Black Stars na Azam FC ambao hao ni watoto wa 2000. Siku hiyo tunakutana na mkubwa mwenzetu, na  wanasimba wote tunatakiwa kuwa kitu kimoja.

Mwanasimba yeyote kuanzania sasa anatakiwa kuomba dua kwa imani yake kwa ajili ya mchezo huo wa utamaduni mkubwa na kugusa maisha yetu ya wanasimba,” amesema Ahmed.

Ameeleza kuwa sasa hawataki kuona wanapoteza tena katika mchezo huo huku wakiwa na matarajio ya kufanya vizuri kwa sababu ya kuwepo kwa kikosi imara na wachezaji kuwafurahisha.

Related Articles

Back to top button