Ligi Kuu

Chilambo nje wiki 4-6

DAR ES SALAAM: BEKI wa kulia wa waoka mikate wa Chamazi Dar es Salaam Azam FC Nathaniel Chilambo anaendelea vema baada ya kupata majeraha ya kuvunjika maungio ya kidole cha mwisho cha mguu wa kulia.

Taarifa iliyotolewa na Azam FC imeeleza kuwa Chilambo alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, dhidi ya Coastal Union majeraha yaliyomfanya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na beki Cheikh Sidibe.

Taarifa imeendelea kueleza kuwa Baada ya vipimo, beki huyo wa kimataifa wa Tanzania, atakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki nne hadi sita.

Aidha imebainishwa kuwa kwa sasa Chilambo yupo chini ya uangalizi wa Mtaalamu wa tiba za viungo wa Azam FC , Romulo Freitas na jopo lake, wanaoendelea kumpa mazoezi tiba kabla ya kurejea dimbani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button