KOCHA msaidizi wa Geita Gold, Mathias Wandiba, amesema timu yake imejipanga vyema kupata ushindi dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu katika Uwanja wa Liti keshokutwa.
Akizungumza na gazeti la gazeti la HabariLEO, Wandiba alisema kuelekea mchezo huo hakuna majeruhi na wachezaji wake wapo katika hali nzuri.
“Timu yetu ipo vizuri na sasa tumejipanga ili kupata ushindi wetu wa kwanza katika Ligi Kuu,” alisema Wandiba.
Naye kiungo wa Geita Gold FC, Deusdedity Cosmas alisema wamejipanga vyema na mechi hiyo.
Aliwaomba mashabiki wao kuendelea kuisapoti timu yao.
Mchezaji huyo wa zamani wa Alliance na Polisi Tanzania alisema ligi ni ngumu lakini wataendelea kupambana wapate ushindi.
Geita ipo katika nafasi ya 12 ikiwa na pointi tatu baada ya michezo minne.
Timu hiyo haijashinda mchezo wowote, imepoteza mechi moja na kupata sare michezo mitatu.




