Ligi KuuNyumbani

Kombe la ubingwa wa 29

LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/2023 imefikia tamati leo kwa Yanga kukabidhiwa kombe la ubingwa baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2=0 katika mchezo wa mwisho kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mabao ya Yanga yamefungwa Fiston Mayele dakika ya 33 huku la pili likifungwa na Yannick Bangala dakika 94.

Mbali na timu za Polisi Tanzania na Ruvu Shooting kushuka daraja, KMC na Mbeya City zitakutana katika michezo miwili kutafuta moja ya kubaki ligi kuu na nyingine kucheza mtoani na timu ya Championship.

Matokeo ya mechi nyingine leo ni kama ifuatavyo:

Mbeya City       0-1   KMC
Mtibwa Sugar   3-1   Geita Gold
Ihefu               2-0   Kagera Sugar
Namungo         1-1   Singida Big Stars
Ruvu Shooting 0-1    Dodoma Jiji
Simba             3-1   Coastal Union
Azam              8-0   Polisi Tanzania

Related Articles

Back to top button