
KIKOSI wachezaji 27 wa Timu ya Taifa ya wanaume U20 kitaingia kambini Okotba 22, 2022 kujiandaa na mashindano ya kufuzu AFCON 2023 Misri Kanda ya Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati(CECAFA).
Kocha Mkuu wa timu hiyo Zubery Katwila amewataja magolikipa kuwa ni Razak Shekimweli, Ramadhan Chuma, Hamad Ubwa na Anthony Remmy.
Mabeki ni Nathaniel Chilambo, Alphonce Mabula, Miraji Abdallah, Pascal Msindo, Elias Lawi, Tariq Abeid, Twalibu Mohamed, AbdulRazak Hamza na Nasry Mkumwila.
Viungo walioitwa ni Joseph Mkele, Hussein Semfuko, Mourice Abraham, Seif Mmad, Hashim Arkan, Omary Buzungu, Vicent Abubakar, Radak Juma, Edwin Balua, Richard Ng’odya na Rashid Muhammed.
Katwila amewataja washumbuliaji kuwa ni Kelvin John, Clement Mzize na Oscar Paul.