Zirkzee aongeza mzuka United

MANCHESTER:MSHAMBULIAJI wa Manchester United Joshua Zirkzee ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha timu hiyo mapema leo Jumanne siku moja kabla ya fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham Hotspur licha yah apo awali kutarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia wa msimu wa 2024/25.
Zirkzee mwenye miaka 23 hajaonekana uwanjani kukitumikia kikosi cha mashetani wekundu tangu Aprili 13 alipotoka nje ya dimba la St James Park akichechemea katika mchezo waliobugizwa bao 4-1 na Newcastle united kisha siku tatu baadae kocha wake Ruben Amorim akanukuliwa akisema ‘hatacheza tena’ msimu huu.
Pamoja na Zirkzee mwenye mabao matatu msimu huu, wachezaji Diogo Dalot na Leny Yoro pia wameonekana katika uwanja wao wa mazoezi wa Carrington leo jumanne huku kuonekana kwa wachezaji hawa kukileta nafuu kwa mashabiki wa Timu hiyo Pamoja na Kocha Amorim kuelekea kwenye mchezo huo wa fainali hapo kesho.
Mapema mwezi huu, Kocha Amorim alionekana kuvurugwa na majeraha ya Yoro mwenye miaka 19, majeraha ambayo aliyapata kwenye mchezo dhidi ya West Ham United wa May 11 kufuatia kuanza vyema msimu kwa beki huyo akisema amepoteza mchezaji wake tegemezi hivyo urejeo wake kikosini ni ahueni kubwa.