Ligi Kuu ZanzibarNyumbani

Zimamoto yaizima Mlandege

MAAFANDE wa kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU), wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mlandege katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo miamba hiyo ilionekana kushambuliana kwa zamu na kwenda
mapumziko kukiwa hakuna aliyeona lango la mwenzake.

Miamba hiyo ambayo inafundishwa na makocha mahiri iliendelea kushambuliana katika
kipindi cha pili na ndipo Zimamoto iliyo chini ya kocha Mohammed Ali Hilal ‘Tedy’ ikaandika
bao lake hilo la pekee kupitia kwa Suleiman Juma dakika ya 53.

Kwa matokeo ya mchezo huo, Zimamoto imefikisha pointi saba ikiwa nafasi ya tano wakati Mlandege ina pointi saba nafasi ya nane ya msimamo wa ligi hiyo ambayo inaongozwa na
KMKM wenye pointi 10.

 

Related Articles

Back to top button