Burudani

Ziggy Marley: Kitabu nilichoandika ni nguvu ya Bob Marley

JAMAICA: NYOTA wa muziki wa Reggae mwenye miaka 56 ambaye ni mtoto wa gwiji la muziki huo Bob na Rita Marley amefichua kuwa kitabu alichoandika kwa ajili ya watoto kilichochewa na nguvu za baba yake.

Akiongea na People, Ziggy amesema: “Kitabu pekee ambacho nimeandika kimechochewa na nguvu za kipekee za baba kwani nguvu nyuma yake ni aina ile ile ya nishati ambayo baba yangu alikuwa nayo.”

Muda mwingi Ziggy hupenda kuwasomea watoto wake vitabu jambo ambalo linatafsiriwa kama kufuata nyayo za Bob Marley aliyekuwa na kawaida kama hiyo wakati wa uahai wake.

“Mke wangu na watoto wetu wadogo huwa na vitabu wakati wa kulala. Nina watoto saba, kwa hiyo wengine ni wakubwa, lakini wanne wangu wa mwisho nilipata nilipokuwa mkubwa kidogo, kwa hiyo tulikuwa tukisoma vitabu vingi pamoja.

“Sasa mdogo wangu ana miaka tisa, na kimsingi, hataki tumsomee tena. Anataka kujisomea mwenyewe.Lakini bado anataka tulale naye kitandani anaposoma!”

Ziggy alimpoteza baba yake alipokuwa na umri wa miaka 12 tu, lakini bado ana kumbukumbu nzuri na wazi za kutumia wakati mzuri na Bob, ambaye alifariki kwa ugonjwa wa saratani mnamo Mei 1981, akiwa na umri wa miaka 36.

Related Articles

Back to top button