Familia

Zari atupa jiwe gizani!

DAR ES SALAAM: MFANYABIASHARA na mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amezua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kueleza tofauti anayoiona kati ya mwanamke tajiri na mwanaume tajiri katika malezi ya watoto.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Zari ameandika kuwa mwanamke anapokuwa na uwezo mkubwa wa kifedha, watoto wake hunufaika moja kwa moja kwa kuishi maisha mazuri, huku mwanaume tajiri akitajwa kuwa chanzo cha kuongezeka kwa idadi ya watoto kutoka kwa wanawake tofauti.

“Mwanamke anapokuwa tajiri, watoto wake hufurahia maisha mazuri, na mwanaume anapokuwa tajiri, watoto wake wata-enjoy undugu usio na mwisho kutoka kwa wanawake tofauti,” ameandika Zari.

Kauli hiyo imepokelewa kwa mitazamo tofauti, ambapo baadhi ya wadau wa mitandao ya kijamii wameunga mkono hoja ya Zari wakisema inalenga kuangazia wajibu wa malezi, huku wengine wakidai kauli hiyo ni ya jumla na haiwakilishi wanaume wote.

Hata hivyo, wapo wanaoamini kuwa ujumbe huo una mlengo wa binafsi, hasa ikizingatiwa kuwa Diamond Platnumz, ambaye ni baba wa watoto wa Zari, ana watoto wengine na wanawake tofauti.

Licha ya tafsiri mbalimbali, kauli ya Zari imeendelea kushika kasi mitandaoni, ikifungua mjadala mpana kuhusu nafasi ya utajiri, majukumu ya wazazi na athari zake katika maisha ya watoto.

Related Articles

Back to top button