Ligi KuuNyumbani

Zahera Kocha Mkuu Polisi Tanzania

TIMU ya Polisi Tanzania imetangaza kuwa imefikia makubaliano na Mwinyi Zahera kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Polisi Tanzania Frank Lukwaro ametoa taarifa ya kufikiwa kwa makubaliano hayo.

“Makubaliano na Kocha Zahera yamefikiwa leo mkoani Kilimanjaro baada ya mazungumzo ya muda mrefu pamoja na tathmini ya kina kwa lengo la kufanya vizuri,” imesema

Kabla ya uteuzi huo Zahera alikuwa huru baada ya kumaliza mkataba wake Yanga Septemba, 2022 akiwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka la vijana na Wanawake.

Polisi Tanzania ilikuwa chini ya Kocha Msaidizi John Tamba tangu Oktoba 18, 2022 baada ya aliyekuwa kocha mkuu Joslin Bipfubusa kutimuliwa kazi Oktoba 26.

 

Related Articles

Back to top button