Ligi KuuNyumbani

Yanga yathibitisha Feisal kutimkia Azam

 

KLABU ya Yanga imethibitisha kumuuza Feisal Salum katika klabu ya Azam kwa dau ambalo imesema halitawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa ya Yanga imesema ilipokea ofa kutoka timu ya Azam ya kumhitaji Feisal.

“Baada ya mazungumzo ya pande zote mbili na kwa kuzingatia matakwa ya kimkataba kati ya klabu na mchezaji, uongozi wa Young Africans Sports Club umefikia uamuzi wa kumuuza mchezaji huyo kwa klabu ya Azam FC,” imesema taarifa hiyo.

Yanga imesema Feisal ataungana na timu yake mpya baada ya makubaliano binafsi na dirisha la usajili kufunguliwa rasmi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button