Ligi KuuNyumbani

Yanga yaendeleza ubabe Ligi Kuu

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Yanga leo imeendeleza ushindi katika mfululizo wa mechi za ligi baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-0 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Yanga ilipata bao lake la kwanza dakika 4 tu ya mchezo likifungwa na Bernard Morrison baada ya kupokea pasi ya Jesus Moloko.

Licha ya Coastal Union kumiliki mchezo kipindi cha kwanza haikufanikiwa kupata bao hadi nusu ya kwanza inamalizika.

Yanga ambayo iliifunga Polisi Tanzania kwa mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kwenye uwanja huo huo ilipata goli la pili dakika 68 likifungwa kwa kicha na Fiston Mayele.

Mayele iliyefikisha mabao mawili hadi sasa amefunga bao hilo akipokea pasi ya kichwa kutoka kwa Djuma Shaban.

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliopingwa uwanja wa Liti mjini Singida, wenyeji Dodoma Jiji wamepokea kichapo cha pili mfululizo baada ya kufungwa mabao 2-1 na Tanzania Prisons.

Mabao ya Prisons yamefungwa na Ismail Mgunda dakika 2 kwa njia ya penalti na Jeremiah Juma dakika 6 wakati bao la Dodoma Jiji limefungwa na Hassan Mwaterema dakika 18.

Related Articles

Back to top button