Ligi Ya WanawakeNyumbani
Yanga, Simba wanawake viwanja tofauti leo

Yanga Princess na Simba Queens leo zinashuka kwenye viwanja tofauti ikiwa ni miongoni mwa michezo 6 ya raundi ya sita Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.
Simba Queens ni wageni wa Amani Queens kwenye uwanja wa shule ya Sekondari Nyangao iliyopo Mtama, mkoani Lindi.
Nayo Yanga itakuwa mgeni wa Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Chuo cha Mkwawa mkoani Iringa.
Katika mchezo mwingine Alliance Girls ni mwenyeji wa Mkwawa Queens kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma utashuhudia Fountain Gate Princess ikiwa mwenyeji wa Baobab Queens.
Vinara wa ligi hiyo JKT Queens itakuwa mwenyeji wa The Tigers Queens kwenye uwanja wa Mej Gen Isamuhyo, Dar es Salaam.