Ligi Ya WanawakeNyumbani

Yanga Princess kujitutumua leo?

LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara(SWPL) inendelea leo kwa michezo miwili kufanyika Dar es Salaam na Mwanza.

Yanga Princess itakuwa mwenyeji wa Baobab Queens kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Fountain Gate Princess ni wageni wa Alliance Girls kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Yanga Princess inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa pointi 22 baada ya michezo 13 wakati Baobab Queens ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 18.

Fountain Gate Princess inashika nafasi ya 3 ikiwa na pointi 29 baada ya michezo 13 wakati Alliance Girls ni ya 5 ikiwa na pointi 20.

Related Articles

Back to top button