Ligi KuuNyumbani

Yanga kurejesha wimbi la ushindi leo?

LIGI Kuu ya soka Tanznaia Bara inaendelea leo kwa michezo miwili  kufanyika Dar es Salaam na Mbeya.

Baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Azam, Yanga itaikaribisha Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga inashika nafasi ya 3 baada ya michezo 3 ikiwa na pointi 7 sawa na Simba iliyopo nafasi ya kwanza na Mtibwa nafasi ya pili lakini inazidiwa idadi ya mabao ya kufunga.

Katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu uliopigwa Juni 29, Yanga ilishinda kwa bao 1-0.

Azam itashuka uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ikiwa mgeni wa Mbeya City.

Mbeya City inashika nafasi ya 7 ikiwa pointi 4 baada ya michezo 3.

Mchezo wa mwisho wa ligi kuu kati ya Mbeya City na Azam ulishuhudia Mbeya City ikishinda kwa mabao 2-1.

Related Articles

Back to top button