Africa

Yanga kuanza hatua ya awali CAFCL

Leo Draw ya Michuano ya Vilabu barani Afrika inafanyika ambapo timu za Tanzania zitafahamu wapinzani wao katika michuano hiyo.

katika Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga na Azam zitaiwakilisha Tanzania huku Coastal Union na Simba zikiwakilisha katika Kombe la Shirikisho.

Yanga, Azam pamoja na Coastal Union zitalazimika kuanza hatua ya awali huku Simba ikianza kwenye hatua ya kwanza.

Ni timu tano pekee kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo hazitoanzia hatua ya awali ambazo ni Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Esperance de Tunis, , Petro Atletico de Luanda na TP Mazembe.

Katika Kombe la Shirikisho timu 12 hazitoanzia hatua ya awali ikiwemo Simba ya Tanzania.

Related Articles

Back to top button