Kwingineko

West Ham yakubali kumsajili Kudus

WAGONGA Nyundo wa London, West Ham United imekubali dili la kumsajili kiungo wa Ajax ya Uholanzi, Mohammed Kudus kwa ada ya pauni milioni 38 sawa na shilingi bilioni 116.7 pamoja na nyongeza.

Kudus mwenye umri wa miaka 23 alifunga mabao matatu wakati wa mchezo wa kufuzu Ligi ya Europa Agosti 24 wakati klabu yake iliposhinda dhidi ya Ludogorets nchini Bulgaria.

Baada ya mechi hiyo mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana alisema huenda mchezo huo ukawa wa mwisho akiwa timu hiyo ya Udachi.

Ripoti zimesema Kudus anatarajiwa kwenda London Agosti 26 kwa ajili ya vipimo vya afya.

Amekuwa akiwindwa na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England majira haya ya kiangazi ikiwemo Brighton ambayo mapema mwezi huu ilifikia makubaliano na Ajax kumsajili lakini haikuweza kukamilisha vipengele binafsi.

Kudus amefunga mabao 27 katika michezo 87 aliyocheza akiwa Ajax tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2020.

Anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na kocha David Moyes katika klabu ya West Ham kutoka Ajax majira haya ya kiangazi kufuatia usajili wa kiungo mwenzake Edson Alvarez kwa dili lenye thamani ya ada ya pauni milioni 35.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button