EPLKwingineko
Webb ataka wachezaji wa zamani kuwa waamuzi

Mkuu mpya wa waamuzi wa Ligi Kuu England Howard Webb amesema anataka wachezaji wa zamani wawe waamuzi wa kulipwa.
Webb aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Mkuu wa Bodi ya waamuzi wa soka la kulipwa England (PGMOL) ana nia ya kukuza kundi la vipaji kwa waamuzi wa Ligi Kuu.
“Ni njia nzuri ya kuendelea kuhusika katika mchezo na tunahitaji kuangalia jinsi tunavyoweza kuwashawishi watu kuwa waamuzi,” amesema Webb.
Ligi Kuu England itarejea Disemba 26 baada ya mapumziko ya michuano ya Kombe la Dunia iliyofikia tamati Disemba 18 kwa Argentina kutwaa ubingwa.